KWA WANAFUNZI WOTE, MALIPO YA ADA NA MALIPO MENGINE

Hii ni kuwajulisha Wanafunzi wote wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaodaiwa madeni ya nyuma “outstanding fees” na ya sasa kuwa wanatakiwa kulipa madeni yao yote.

Pia mnajulishwa kuwa, kwa malipo ya ada na malipo mengine “direct cost” kwa muhula wa pili ambao ulianza tarehe 17 Machi 2018, mnatakiwa kulipa angalau kuanzia shilingi laki tatu (300,000/=) ili muweze kusajiliwa.

Mwisho wa kufanya usajili ni tarehe 9/04/2018.

Wanafunzi wote mnahimizwa kutumia muda huu vizuri.

 

Imetolewa na:

Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo

Mipango, Fedha na Utawala