UDOM YAANZA KUHAMASISHA WANAFUNZI WA KIKE KUPENDA MASOMO YA SAYANSI


  • 1 year
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia mradi WA HEET kipo kwenye program ya uhamasishaji kwa wanafunzi wa kike waliopo shule za sekondari ili waweze kuyapenda na kuyasoma masomo ya Sayansi ( STEM) discipline.

Uhamasishaji huu unalenga kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwenye Jamii kwamba masomo ya Sayansi ni magumu na kwamba yanaweza kusomwa na watoto wa kiume zaidi kuliko wanawake.

Licha ya uhamasishaji huo, program hii ina lengo la kuzitangaza kozi mbalimbali zinazotolewa katika chuo Kikuu cha Dodoma kwa ngazi ya Shahada katika taaluma ya STUH (yaan Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati) katika Ndaki za Sayansi Asilia na Hisabati, Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu, Ndaki ya Sayansi Za Ardhi na Uhandisi Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa Pamoja Shule Kuu Uuguzi na Afya ya Jamii

Program hii inafanyika katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Morogoro na Manyara

Comments
Send a Comment