WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA UDOM


  • 1 year
  • Office of The Vice Chancellor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Faustine Mkenda(Mb) ametembelea Chuo Kikuu cha Dodoma leo tarehe 28 Aprili, 2023. Mhe. Waziri aliongozana na Prof. Carolyne Nombo – Katibu Mkuu; pamoja na Prof. James Mdoe – Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Lengo kuu la ziara yao ilikuwa ni kujionea changamoto ya maji Chuoni. Mheshimiwa Waziri na ujumbe wake walitembelea Bweni Namba G katika Ndaki ya Elimu na kujionea jinsi changamoto ya maji inavyoathiri wanafunzi. Mhe. Waziri aliahidi kufanyia kazi changamoto hiyo kadiri itakavyowezekana.
 

Comments
Send a Comment