KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UBUNIFU DODOMA


  • 1 year
  • Directorate of Research, Publications and Consultancy

Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kivutio kwa viongozi na wananchi kupitia bunifu mbalimbali za teknolojia katika maadhimisho ya wiki ya ubunifu kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma kuanzia tarehe 24-28 Aprili, 2023

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la UDOM Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka ameeleza kuridhishwa na bunifu mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa UDOM kwa kuwa zinatatua moja kwa moja changamoto za jamii

Aidha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri kwa Umma amewataka wabunifu hao kuziongezea tija bunifu zao ili ziweze kuingia katika soko la ushindani

Comments
Send a Comment