UDOM YATOA ELIMU YA MAZINGIRA-NTUKYA


  • 11 months
  • Geography and Environmental Studies

Chuo kikuu cha Dodoma kupitia Idara ya Jiografia na Mazingira Ndaki ya Insia na Sayansi ya Jamii inaadhimisha siku ya Mazingira Duniani kuanzia tarehe 29 Mei 2023 mpaka siku ya kilele tarehe 5 Juni 2023

Idara imeandaa kazi za utoaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka chuo ikiwemo Kata ya Ngong'onha, Kata ya Ntyuka na kata ya Makulu. Tarehe 30 ilikuwa Ngong'onha Tarehe 31 ilikuwa ni Ntyuka

Pia Idara ya Jiografia na Mazingira imeshirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais kusafisha jiji la Dodoma ambapo tarehe 1/6/2023 walikuwa Shule Sekondari Kiwanja cha Ndege Sekondari na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo

Tarehe 5 Juni 2023 itakuwa ni kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambapo Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango atakuwa Mgeni Rasmi na maadhimisho yatafanyika Makulu- Dodoma

Comments
Send a Comment