KAMPENI ZA UCHAGUZI UDOSO 2023/24 ZAFUNGULIWA


  • 11 months
  • Directorate of Students Services

Leo tarehe 26 Mei, 2023 Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka amefungua rasmi Kampeni za Uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kampeni hiyo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka aliwaeleza wagombea katika nafasi mbalimbali mambo ya kuzingatia wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kutumia lugha ya staha katika kampeni. Aidha, alisisitiza kufanya kampeni za amani na utulivu na aliipongeza Tume ya Uchaguzi kwa kazi nzuri ya kusimamia mchakato wa zoezi la uchaguzi.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Wineaster Anderson alitoa aliwapongeza Tume ya Uchaguzi kwa kuendesha zoezi la kupata wagombea wenye sifa kwa umakini mkubwa na kuwaasa wagombea kuendesha kampeni kwa amani na utulivu.

Uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dodoma unatarajiwa kufanyika tarehe 28 Mei, 2023 ambapo wanafunzi watapata fursa ya kumchagua rais wa Serikali ya wanafunzi, Magavana na Manaibu Gavana, Wabunge, Wawakilishi wa Madarasa na Viongozi wa Mabweni.

Comments
Send a Comment