MAFUNZO KWA VIONGOZI WAPYA WA UDOSO 2023/24 KIBAHA-PWANI


  • 11 months
  • Directorate of Students Services

Menejimenti ya Chuo kikuu cha Dodoma imewezesha mafunzo ya uongozi kwa viongozi wapya wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO 2023/24) ambayo yanafanyika katika Shule Kuu ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (Mwl. Julius Nyerere Leadership School) iliyopo Kibaha-Pwani. Mafunzo haya yanafanyika kwa siku mbili tarehe 2-3 Juni 2023 .

Wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo Rasi wa Shule kuu ya Uongozi Prof. Marcelina Chijoriga ameshukuru Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuwaleta wanafunzi mahali hapo na ameahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha na ameahidi kuwa hadi mafunzo kumalizika viongozi watakuwa wameimarika kwa ajili ya kuongoza vyema kwa maendeleo ya Chuo na Taifa kwa ujumla

Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe.Remidius Mwema Emmanuel ambaye pia alikuwa mwezeshaji wa mada katika mafunzo hayo.
Aidha katika mafunzo hayo zipo mada kadha wa kadha zitakazowasilishwa na wawezeshaji mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,taasisi na watu mashuhuri wenye uzoefu katika masuala ya uongozi zitakazo enda kuwajenga wanafunzi hawa viongozi.

Comments
Send a Comment