MTENDAJI MKUU WA BENKI YA NMB ATEMBELEA UDOM


  • 11 months
  • Office of The Chancellor

Mtendaji Mkuu wa Benki ya  NMB-TANZANIA Bi.Ruth Zaipuna ametembelea Chuo Kikuu cha Dodoma tarehe 19 Mei, 2023 kwa lengo la kuzungumza na Chuo kuhusu fursa mbalimbali za benki ya NMB.

Fursa hizo ni pamoja na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka alimshukuru sana Bi. Ruth Zaipuna kwa kushirikisha Chuo Kikuu cha Dodoma fursa mbalimbali zinazipatikana katika Benki ya NMB na kwamba Chuo kitazifanyia kazi.

Mtendaji Mkuu wa NMB aliambatana na viongozi mbalimbali wa benki hiyo wa ngazi ya tawi, mkoa, kanda na makao makuu.

Comments
Send a Comment