MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA DODOMA MGENI RASMI STICE 2023


  • 10 months
  • Office of The Vice Chancellor

Reposted from @costech_tz #STICE2023 Mgeni rasmi wa Kongamano la 8 la Sayansi, Teknolokojia na Ubunifu- STICE, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka akikagua Mabanda ya Maonesho, Leo tarehe 16 Juni 2023 katika Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika ukumbi wa JNICC - Jijini Dar es salaam.

Prof. Kusiluka pia amepata nafasi ya kukutana na kupatiwa maelekezo ya mfumo wa umeme bila kutumia nyaya (wireless) inayotumika kutibu magonjwa kwa kutumia masafa ya sauti na kipimo cha cremonia toka kwa kwa mwanafunzi Tanya Gorecha wa Shule ya Genesis OysterBay, anayesoma kidato cha kwanza, katika kongamano la nane la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STICE)lililofanyika kwa siku tatu (3) kuanzia tarehe 14 - 16 Juni 2023 .

Aidha, Mgeni ramsi huyo alipokelewa na kutembelea Mabanda hayo akiwa na Mwenyeji wake ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara ya Elimu, Menejimenti na Wafanyakazi wa COSTECH.
 

Comments
Send a Comment