BONANZA LA MICHEZO KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU


  • 10 months
  • Directorate of Students Services

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala Prof.Wineaster Anderson ameshiriki katika Bonanza la michezo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu Chuo Kikuu cha Dodoma katika Viwanja vya Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu. Bonanza hilo lililofanyika tarehe 25. 06.2023, lililohusisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, shindano la kunywa soda, kuvuta kamba, mpira wa kengele kwa wasioona, mchezo wa Draft, mchezo wa kukimbia na yai na kucheza bao.

Lengo Bonanza hili ni kuwajengea wanafunzi wenye mahitaji maalum uwezo wa kushiriki katika michezo mbalimbali kwa nia ya kuimarisha afya ya akili na mwili.

Akizungumza na wanafunzi hao, Prof. Wineaster Anderson alisema kuwa wanafunzi wasio na mahitaji maalumu wanapaswa kujali wenzao walio na mahitaji maalum kwa kuwapa ushirikiano wanaouhitaji ili waweze kutimiza malengo yao ya kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma. Alieleza kuwa, Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma itaendelea kuwapa ushirikiano wote wanaouhitaji ili waweze kutimiza malengo yao ya kupata elimu ya juu.

Aidha, Prof. Anderson aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapatia wanafunzi wenye mahitaji maalum msaada wa vifaa vya kuwawezesha kurahisha maisha yao ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma kama vile bajaji na vifaa vya kujifunzia.

Comments
Send a Comment