BONANZA LA WAFANYAKAZI CHUO KIKUU CHA DODOMA


  • 10 months
  • Directorate of Administration and Human Resource Management

Wanafunzi wamehimizwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu katika mitihani kitendo kinachoweza kupelekea kufukuzwa chuo.

Hayo yameelezwa leo tarehe 27 Juni, 2023 na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo(IDS) Prof. Odass Bilame alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa taasisi hiyo katika semina elekezi kwaajili ya mitihani ya muhula wa pili inayotarajiwa kuanza tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu. Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwakumbusha wanafunzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo juu ya kufuata taratibu na sheria za mitihani

Katika semina hiyo wanafunzi pia walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu sheria na kanuni za mitihani.

Mwisho, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za maendeleo ( IDS ) aliipongeza Serikali ya wanafunzi katika taasisi hiyo inayoongozwa na Gavana Enock Genzes kwa ubunifu huo na kwa kuhamasisha wanafunzi waweze kushiriki katika tukio hilo ili waweze kuzijua kanuni na sheria za mitihani.

Comments
Send a Comment