TUME YA UCHAGUZI UDOSO 2023/24 YAPONGEZWA


  • 10 months
  • Directorate of Students Services

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka ameipongeza Tume ya Uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi UDOSO-EC kwa kazi nzuri ya kufanikisha uchaguzi wa viongozi wa Serikali ya Wanafunzi kwa mwaka 2023/24 ambapo walitunikiwa vyeti vya kutambua kazi nzuri waliyofanya ya kuendesha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa katika hafla iliyofanyika tarehe 19.06.2023.

Akizungumka katika hafla ya kuwapongeza viongozi hao, Makamu Mkuu wa Chuo alieleza kuwa uchaguzi huo ulifanyika katika hali ya usalama, utulivu na amani kutokana na ushirikiano wa Tume katika kuweka mipango na mikakati thabiti ya kuendeshea uchaguzi kwa haki na amani.

Makamu Mkuu wa Chuo aliwapongeza viongozi waliochaguliwa huku akiwaasa kutambua dhamana waliopewa ya kuongeza wanafunzi zaidi ya 32,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Alieleza kuwa Manejimenti na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wako tayari kushirikiana na uongozi mpya wa UDOSO katika kufanikisha majukumu yao ambayo yamebebwa na misingi mikuu mitatu “Sheria, Kanuni na Taratibu. Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo aliwapongeza uongozi waliomaliza muda wake kwa kwa kazi nzuri sana ya mfano wa kuigwa. Aliwaasa kushirikiana na viongozi wapya ili waendeleze yale mazuri waliyofanyika katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wao.

Katika hafla hiyo Makamu Mkuu wa Chuo alimpongeza Mkurugenzi wa Huduma kwa wanafunzi na ofisi yake chini ua uongozi madhubuti ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Mipango, Fedha na Utawala Prof. Wineaster Anderson kwa usimamizi mzuri wa Uchaguzi huo.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo- Taaluma, Utafiti na Huduma kwa Jamii Prof. Razack Lokina na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala Prof. Wineaster Anderson ambao waliipongeza Tume kwa kuendeshea zoezi la Uchaguzi kwa weledi mkubwa. Vilevile Mabalozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma

“UDOM Ambassadors walipongezwa kwa kazi nzuri ya kutangaza shughuli za Chuo Kikuu cha Dodoma ikiwa ni pamoja na zoezi zima ya uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi 2023/24.
 

Comments
Send a Comment