UDOM KUBORESHA UZALISHAJI WA VIAZI VIKUU KUSINI


  • 4 months
  • The University of Dodoma

Watalaamu toka Idara ya Bailojia ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wanatarajia kufanya utafiti wa kuwezesha matumizi ya Teknolojia katika kuboresha uzalishaji wa viazi vikuu nchini.

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa mradi huo Dkt. Gladness Elibarick Temu kutoka UDOM mara baada ya kupokea hundi yenye thamani ya TZS 118.5 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kutoka Kituo cha Stadi za Teknolojia cha Afrika (Africa Centre for Technology Studies) cha jijini Nairobi nchini Kenya kwa usimamizi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Mradi huo ambao unaotekelezwa na Idara ya Bailojia kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Mazao (TARI) cha wilayani Kibaha mkoani Pwani utafanyika kuanzia Januari 2024 hadi Juni 2025 na unatarajiwa kuleta matokeo chanya katika kuboresha zao la viazi vikuu katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani.

Comments
Send a Comment