UDOM YAZINDUA MAFUNZI YA MUDA MFUPI YA AKILI UNDE (AI)


  • 6 hours
  • The University of Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohamed Abdallah, leo Jumatatu tarehe 15 Septemba 2025, amezindua rasmi Mafunzo ya Muda Mfupi ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) yanayoratibiwa kupitia Mradi wa The AfriAI Lab. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Afrika Mashariki, uliopo katika Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu (CIVE), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Mohamed amekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini, hususani katika eneo la matumizi ya Akili Unde (AI).

Kwa upande wake, Prof. Ismail J. Ismail, Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo na Rasi wa Ndaki ya Biashara na Uchumi (CoBE), amesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu katika kuendeleza matumizi ya teknolojia za AI nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwajengea washiriki uelewa wa kina kuhusu fursa na matumizi ya AI katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi, na hivyo kuchochea mageuzi ya kidijitali kwa maendeleo endelevu ya taifa.

Comments
Send a Comment