UDOM KUJENGA KAMPASI NJOMBE


  • 4 months
  • Office of The Vice Chancellor

Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) kinatarajia kufungua kampasi mkoani Njombe.

Hayo yamebainika kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kilichoongozwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka tarehe 22 Disemba 2023, ambapo kilijadili uanzishwaji wa kampasi hiyo.

Akiwasilisha mpango wa utekelezaji wa chuo hicho, Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka amesema kiasi cha dola za kimarekani mil 8, ambazo ni sawa na shilingi bilioni 18 za kitanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi na uanzishwaji wa kampasi hiyo.

Prof Kusiluka ameongeza kuwa, programu zitakazotolewa katika kampasi hiyo zitakuwa na tija kwa maendeleo ya jamii ya Njombe na taifa kwa ujumla.

Comments
Send a Comment