UDOM YAPIGA HATUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEET KATIKA MATUMIZI YA TEHAMA


  • 1 month
  • Office of the Deputy Vice Chancellor Academic, Research and Consultancy

Chuo Kikuu cha Dodoma kimepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa matumizi ya TEHAMA kupitia mradi wa HEET ambapo asilimia 90 ya utekelezaji imekamilika.

Hayo yameelezwa katika kikao cha waratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kinachohusisha taasisi zote zinazotekeleza Mradi huo kinachofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Februari 2024, jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msoffe, alieleza kuwa, lengo la kikao hicho ni kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi kutoka taasisi nufaika ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kutafakari kwa pamoja mwenendo wa utekelezaji wa mradi, changamoto zilizopo na kutafuta namna bora na rahisi za kutatua changamoto hizo pamoja na kukumbushana umuhimu wa kuzingatia taratibu za Benki ya Dunia na taratibu za nchi katika utekelezaji wa Mradi.

Akiwasilisha utelekezaji wa Mradi huo katika Chuo Kikuu cha Dodoma, mwakilishi wa Mratibu wa Mradi, Prof. Godlisten Kombe, alieleza utekelezaji wa Mradi wa HEET kwa UDOM na hatua zake kwa kila kipengele ikiwa ni pamoja na maendeleo ya majenzi kampasi ya Dodoma, ujenzi wa kampasi mpya ya Njombe, mafunzo ya muda mrefu na mfupi, uishaji wa mitaala, na matumizi ya TEHAMA katika shughuli mbalimbali za taasisi za kitaaluma pamoja na zile za uendeshaji. Aidha, UDOM imejenga uwezo katika masuala ya utafiti na ubunifu, kujenga uwezo katika katika utendaji kwenye masuala ya jinsia, uundwaji wa Kamati za kishauri za kitasnia yaani industrial Advisory Committees pamoja na makubaliano yaliyoingiwa kati ya UDOM na waajiri.

Kikao hicho kilihudhuriwa na waratibu kutoka taasisi zote zinazotekeleza mradi wa HEET na wataalamu wa vipengele mbalimbali vya mradi, pamoja na Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi wa HEET kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Comments
Send a Comment