VIONGOZI WAPYA UDOSO 2024/25 WAANZA MAFUNZO YA UONGOZI KIBAHA


  • 1 month
  • The University of Dodoma

Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma wameanza mafunzo ya Uongozi ambayo yanayofanyika katika Shule Kuu ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (Mwl. Julius Nyerere Leadership School) iliyopo Kibaha-Pwani. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 6-8 Juni 2024 .

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.Julius Mtatiro amewapongeza wanafunzi hao kwa kuchaguliwa kuwa viongozi kati ya wengi na amewataka viongozi hao kuzingatia mafunzo hayo kwani sio vyuo vyote vinawapa nafasi wanafunzi kupata mafunzo hayo.

Kwa upande mwingine Mhe.Mtatiro ni mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia atatumia uzoefu wake katika kuwajenga wanafunzi hao.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi Bi. Rhoda Aroko ameshukuru uongozi wa UDOM kutoa nafasi nyingine ya kuwawezesha viongozi kupata mafunzo ambayo yatawajenga katika kufuata Sheria,taratibu,kanuni na miongozo ili kufikia malengo.

Aidha, Rasi wa Shule Kuu ya Uongozi Prof. Marcelina Chijoriga ameshukuru Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuwaleta tena viongozi wa UDOSO mahali hapo na ameahidi watawajenga vyema viongozi hao kupitia mada mbalimbali zitakazofundishwa katika mafunzo hayo.

Comments
Send a Comment