WANATAALUMA UDOM WAJENGEWA UWEZO WA UANDISHI WA MIRADI NA TAFITI


  • 1 week
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Shule kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa (SoMD) kimeanza mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo wanataaluma na watafiti wake katika nyanja za Uandishi wa Miradi na Tafiti, pamoja na Mbinu za kuomba Ufadhili wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Mafunzo hayo yanafanyika katika ukumbi wa Rafiki Hotel jijini Dodoma kuanzia 22 hadi 26 Aprili 2025.

Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha washiriki kuboresha uandishi wa maandiko ya kisayansi na miradi ya utafiti, sambamba na kuwapa mbinu na maarifa ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi ya kuvutia wafadhili wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi Prof Razak Lokina amesema mafunzo hao yatawezesha kuwajengea uwezo kwa watafiti ili waweze kuandika miradi mikubwa ambayo inaweza kuvutia wafadhili wengi kuweza kiufadhili


Naye Kaimu Amidi Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa Dkt. Shakilu Jumanne, amesema mafunzo hayo yataongeza tija kwa kuwawezesha wahusika kutekeleza tafiti zenye kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya.

Mafunzo hayo yanashirikisha wanataaluma kutoka idara mbalimbali kutoka Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa.

Comments
Send a Comment