USHIRIKIANO WA UDOM NA OSLO WAZAA MAFUNZO YA UTAFITI
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia mradi wa Elimu ya Shahada ya Uzamivu katika Kuimarisha Sekta ya Afya Nchini Tanzania (DOCEHTA) unatekelezwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Oslo nchini Norway, umeanza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki kutoka taasisi mbalimbali za afya na elimu hapa nchini kuhusu namna ya kufanya tafiti. Mafunzo hayo yalianza Jumatatu tarehe 28 Aprili 2025.