UDOM YAIFIKIA SEKONDARI YA DKT. SAMIA DODOMA
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Kurugenzi ya Huduma za Maktaba, wametembelea Shule ya Sekondari Dkt. Samia iliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa kuwajengea wanafunzi ari ya kusoma vitabu pamoja na kuwahamasisha kujiunga na UDOM.
Tukio hili liimefanyika tarehe 30 Aprili, 2025 likihusisha ugawaji wa zawadi mbalimbali kama vile vitabu, kalamu na vipeperushi.