UDOM KUSHIRIKIANA NA NMB
Chuo Kikuu cha Dodoma kimeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya NMB katika eneo la ukuzajii wa Teknolojia za Kidigitali.
Hati ya Mashirikiano imesainiwa leo tarehe 2 Mei 2025 katika hafla fupi ya utiaji saini iliyofanyika katika Ndaki ya Sayansi za Komputya na Elimu Angavu (CIVE) Ukumbi wa Afrika Mashariki na kushuhudiwa na wajumbe wa pande zote mbili.
Utiaji saini huo umefanywa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka na Afisa Mkuu Rasilimali watu wa Benki ya NMB Bw. Emmanuel Akonaay.
Makubaliano ya mkataba huo yanalenga kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuibua na kuendeleza vipaji mbalimbali kwenye upande wa TEHAMA, kufanya Majaribio mbalimbali ya Teknolojia kwenye masuala ya kifedha, kuboresha mifumo ya kidigitali chuoni, kutoa Elimu ya fedha na kuanda programu maalumu za kukuza uwezo kutoka kwa watalaamu mbalimbali.