WANAFUNZI WATATU WA PhD UDOM WAIBUKA WASHINDI KWENYE WASILISHO LA TAFITI
Wanafunzi Watatu wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), leo tarehe 25 Julai, 2025 wameibuka washindi katika Shindano la Uwasilishaji Tafiti kwa muda wa dakika tatu (3 Minutes Research Competition), lililofanyika
UDOM. Shindano hili limeandaliwa na Kurugenzi ya Shahada za Uzamili UDOM kwa kushirikiana na Mradi wa DOCEHTA.
Mshindi wa kwanza katika mchuano huo kutoka UDOM ameibuka na zawadi ya Shilingi 500,000/-. Awamu ya pili ya shindano hilo itafanyika tarehe 1 Agosti, 2025 na itahusisha washiriki kutoka vyuo vitatu ambavyo ni UDOM, MUHAS na Chuo Kikuu cha Oslo cha nchini Norway. Mshindi katika shindano hilo atazawadiwa Shilingi 1,000,000/-
Shindano hilo lilifunguliwa na Prof. Godlisten Kombe, akimwakilisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi na kusimamiwa na Majaji watatu ambao ni, Kaimu Mkurugenzi wa Tafiti, Machapisho na Ushauri Elekezi Prof. Pendo Kasoga, Kaimu Mkurugenzi wa Shahada za Uzamili Dkt. Julius Ntwenya na Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uuguzi na Afya ya Jamii UDOM, Dkt. Walter Milanzi.