UDOM KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA HENAN CHA NCHINI CHINA


  • 1 day
  • The University of Dodoma

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Henan (HAUST) cha nchini China, leo tarehe 21 Agosti, 2025 wamesaini Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya ufundishaji, Sayansi, Taknolojia, Afya na Kilimo.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Baraza la Chuo, Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka amesema, mashirikiano hayo yataleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo na Afya hapa nchini, kwani yatahusisha matumizi ya teknolojia za kisasa.

"Tunahitaji kutumia teknolojia katika kilimo ambayo itatusaidia kuzalisha hata katika mazingira yasiyokuwa na mvua za kutosha," aliongeza Prof. Kusiluka.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa, Chuo Kikuu cha HAUST Prof. Guo Xiangchui amesema, wao wanatumia vifaa bora pamoja na Teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence) katika Kilimo (Agricultural Engeneering) na wako vizuri katika Sayansi ya Tiba (Medical Science) pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mashirikiano hayo yanatarajiwa kuongeza chachu katika uanzishwaji wa tawi jipya la UDOM mkoani Njombe, ambalo litajikita zaidi katika ufundishaji masomo ya Kilimo na Biashara.

Comments
Send a Comment