BARAZA LA CHUO LAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA UJENZI WA MIRADI


  • 9 hours
  • The University of Dodoma

Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), leo tarehe 1 Septemba 2025, limefanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea kutekelezwa na Chuo hicho.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni:
• Mradi wa ujenzi wa Maabara ya Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati (CNMS),
• Ujenzi wa Madarasa ya Ndaki ya Sayansi za Ardhi na Uhandisi (CoESE) kupitia mradi wa HEET,
• Ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita milioni moja katika Ndaki ya Elimu,
• Ujenzi wa Maabara ya Atomia katika Shule Kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa (SoMD), pamoja na
• Ujenzi wa Kituo cha Polisi Chimwaga.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Rwekaza Mukandala, aliwataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati na kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika mikataba ya ujenzi.

Prof. Mukandala alisisitiza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutaimarisha kwa kiwango kikubwa mazingira ya kujifunzia na kufundishia, kuongeza ufanisi wa utoaji huduma, na hivyo kuendeleza mchango wa UDOM katika maendeleo ya Taifa.

21h
Comments
Send a Comment