MKANDARASI WA KAMPASI YA UDOM NJOMBE APEWA SIKU 365 KUKAMILISHA UJUMBE
Mkandarasi aliyeshinda Zabuni ya Ujenzi wa Majengo Kampasi ya UDOM Njombe; DIMETOCLASA REALHOPE LIMITED , ameaswa kukamilisha Mradi wa Kampasi Mpya ya Njombe ndani ya siku 365 kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Ujenzi uliosailiwa Leo Jumatatu kwenye Ukumbi wa Ofisi za Makao Makuu ya mkoa wa Njombe.
Akizungumza wakati wa Utiaji Saini, Mkataba huo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka, ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma kwa maamuzi ya kumtumia Mkandarasi mzawa, na kwamba uongozi wa Mkoa unaimani kubwa kwamba ataitendea haki fursa hiyo adhimu.
"Tunaishukuru Serikali kwa kumuamini Mkandarasi Mzawa, na Mshauri Elekezi wa Mradi wote wazawa kusimamia Mradi huu Mkubwa wa takribani Bilioni 20.” Alisema
Aidha, amesisitiza Mradi huo ni mkubwa sana kutekelezwa kwa muda ulioelezwa na anaamini ni mradi ambao upo ndani ya uwezo wa wakandarasi wa Kitanzania" Alisisitiza Mtaka.
Naye; Mwenyekiti wa Baraza la Chuo la Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Rwekaza Sympo Mukandala, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Suluhu Hassan, kwa maamuzi aliyoyafanya ya kuhakikisha angalau kila Mkoa unakuwa na Chuo Kikuu Kimoja.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka, amezitaja fursa mbalimbali ambazo wakazi wa Njombe na Mikoa ya jirani wataweza kunufaika nazo I baada ya kumaliza Ujenzi wa tawi la UDOM Njombe ikiwemo: Vijana kuelimika, kuongezeka kwa fursa nyingi za biashara na kukuza uchumi wa Njombe kiujumla.
Kwa upande wake; Mkurugenzi wa Kampuni ya DIMETOCLASA REALHOPE LIMITED, Bw. Dickson Mwaipopo, ametoa hofu kwa wananchi kuwa mradi huo utakelezwa kwa wakati kadri ya muda ulivyopangwa.