UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI UDOSO 2025/26
Naibu Makamu Mkuu Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Prof. Razack Lokina Siku ya leo tarehe 9 Mei, 2025 katika Ukumbi wa Auditorium CIVE amezindua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma ambazo hufanyika kila Mwaka.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hizo Prof. Razack Lokina ametoa wito kwa wagombea kuwa na uchaguzi wa amani na utulivu.
" Hairuhusiwi kufanya Kampeni kwa lugha yoyote isiyofaa mkumbuke haya ni maisha ya uchaguzi baada ya hapa mtarudi maisha ya siku zote " Alisisitiza Prof. Lokina
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma Bi. Rhoda Aroko amewapongeza Wanafunzi wote waliothubutu kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi na amewataka wagombea hao kuzingatia kanuni na miongozo yote iliyowekwa ili kwenda sawia na katiba ya UDOSO.
Akiwasilisha Taarifa ya Uchaguzi Mwenyekiti wa Tume Bi. Shamimu Mganga ameshukuru uongozi wa chuo kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanaupata toka mchakato ulipoanza.
Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo ni Uraisi, Makamu wa Rais, Gavana, Naibu Gavana na Ubunge