JWTZ YAFANYA ZIARA YA KIUTAFITI UDOM
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania( JWTZ) siku ya leo tarehe 15 Mei 2025 limefanya ziara ya Kiutafiti lengo ikiwa ni kupata uzoefu kuhusu namna bora ya uandaaji wa Wahadhiri ambao wanakuwa na sifa za kuweza kufundisha vyuo mbalimbali vya kijeshi nchini.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Prof. Razack Lokina amesema namna bora ya kupata Wahadhiri wenye sifa kwanza ni lazima wawe Waadilifu na uwezo wa kuandika Machapisho ya kutosha yenye hadhi ya Kitaifa na kimataifa.